Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-USALAMA

Zaidi ya raia 50,000 wazingirwa na IS katika mji wa Raqqa

Baada ya Mosul kukombolewa siku ya Jumapili Julai 9 na vikosi vya Iraq, kundi la Islamic State linendelea kushikilia ngome yake ya Raqqa, nchini Syria. Vita vya kuukomboa mji huu vilizinduliwa tangu majira ya joto mwaka jana.

YPG yapambana katika mita ya Raqqa, Julai 3, 2017.
YPG yapambana katika mita ya Raqqa, Julai 3, 2017. REUTERS/Goran Tomasevic TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa makundi ya Waarabu wa Kikurdi kutoka makundi ya waasi ya Syria unakaribia mji wa kale katika siku za hivi karibuni kutokana na msaada wa Marekani. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kati ya raia 30,000 na 50,000 wamezingirwa na kundi la Islamic State.

Raia hawa walikua 300 000 mwaka 2014 na 100 000 mwishoni mwa mwezi Juni na chini ya 50 000 mapema mwezi Julai. Idadi ya watu waliokwama katika mji wa Raqqa inaendelea kupungua lakini bado iko juu sana kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).

Tofauti na Mosul, hakuna eneo lililotengwa mjini Raqaa kwa minajili ya kuwafikisha raia msaada wa kibinadamu, na hivo kuacha raia bila uwezekano wowote wa kukimbia mapigano katikati ya mji, na hivyo kukabiliwa na uhaba ewa maji safi, madawa na chakula.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi limeweza kufungua eneo jipya kwa minajili ya kuwafikisha raia vifaa muhimu karibu na mji huo. Eneo hilo linaunganisha Aleppo na mpaka wa Uturuki, na hupita kama kilomita thelathini kaskazini ya mji wa Raqqa, sehemu ambapo kunapatikana kambi ya Ain Issa, yenye wakimbizi 20 000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.