Pata taarifa kuu

Hali ya wasiwasi yatanda kabla ya Jukwaa la Davos kuanza

Kwa mikutano hii ya kwanza ya uso kwa uso ya msimu wa baridi tangu janga la Uviko-19, baada ya toleo lililopunguzwa lililoandaliwa mwezi Mei mwaka uliyopita, Jukwaa la Uchumi Duniani la Davos ambalo linafunguliwa Jumanne Januari 17 linafanyika katika muktadha wa wasiwasi mkubwa juu ya hali ya ulimwengu.

Takriban wakuu hamsini wa nchi na serikali, na baadhi ya viongozi wa biashara wakubwa 1,500 na wadau katika masuala ya uchumi, wanatarajiwa mjini Davos.
Takriban wakuu hamsini wa nchi na serikali, na baadhi ya viongozi wa biashara wakubwa 1,500 na wadau katika masuala ya uchumi, wanatarajiwa mjini Davos. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Karibu kila mwaka kwa wakati mmoja kwa zaidi ya nusu karne, Jukwaa la Uchumi Duniani ambalo linahudhuriwa na wanasiasa, wafanyabiashara, watu mashuhuri na wanaharakati wakubwa wa masuala ya kijamii - maarufu kama jukwaa la Davos -wanakutana kuanzia Jumanne hii katika kituo kidogo cha mapumziko cha Davos, katika Alpen ya Uswisi. Takriban marais na viongozi wa Serikali hamsini wanatarajiwa, watu mashuhuri1,500 na wadao katika masuala ya uchumi, wakiwemo wakurugenzi wa benki kuu na wakuu wa taasisi za kimataifa wanatarajiwa katika mkutano huo. Bila kutaja wawakilishi wa mashirika ya kiraia na ulimwengu wa utamaduni.

Kwa toleo hili la 53, Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) limechagua mada 'Kushirikiana katika ulimwengu uliogawanyika'. 

"Migogoro ya kiuchumi, kimazingira, kijamii na siasa za kilimwengu inazidi kutanuka na kujichwanya, huku ikiandaa mustakabali mgumu sana na usio na uhakika. Mkutano huu wa kila mwaka wa Davos lazima ujaribu kuhakikisha kuwa viongozi hawasalii kunasa kwenye akili hii ya migogoro" , amesema mwanzilishi wa jukwaa hilo, Klaus Schwab, huku akiwaambia waandishi wa habari kwamba dunia ipo kwenye mkwamo ambao lazima viongozi wa dunia waukwamue.

Kongamano hilo linafanyika wakati dunia ikiwa kwenye mfadhaiko mkubwa unaodhihirika kupitia mfumko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu, mgogoro wa nishati na kuharibika kwa mfumo wa usambazaji bidhaa duniani kulikosababishwa na vita nchini Ukraine na kuzuka upya kwa maambukizo ya virusi vya Corona nchini China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.