Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-USALAMA

Jeshi la Iraq laanzisha mashambulizi dhidi ya IS karibu na Kirkuk

Vikosi vya Iraq vimeanzisha Alhamisi hii operesheni ya kurejesha kwenye himaya yao mji wa Hawija, magharibi mwa mji wenye utajiri wa mafuta wa Kirkuk, baada ya kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State.

Vikosi vya jeshi la Iraq vimeanzish amashambulizi ya kuokomboa mji wa Hawija kutoka mikononi mwa IS
Vikosi vya jeshi la Iraq vimeanzish amashambulizi ya kuokomboa mji wa Hawija kutoka mikononi mwa IS MOHAMED EL-SHAHED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Hawija ni moja ya maeneo yaliodhibitiwa na kundi la Islamic state mwaka 2014.

Operesheni hii iliyiotangazwa na Waziri Mkuu wa Iraq Haïdar al Abadi, inakuja siku nne kabla ya kura ya maoni juu ya uhuru wa Kurdistan nchini Iraq, iliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu kaskazini mwa Iraq, hasa katika mji wa Kirkuk.

Abadi ametoa wito wa kufuta kura hiyo inayotambuliwa na Mahakama Kuu kuwa ni "kinyume na Katiba" ya nchi ya Iraq.

Mji wa Hawija, unapatikana kaskazini mwa Baghdad, na ni mojawapo ya maeneo ya mwisho ambayo bado yanadhibitiwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS). Mapigano mengine ya kujitoa mikononi mwa kundi la IS yanaendelea upande wa mashariki wa mpaka wa Syria katika Bonde la Firate.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.