Pata taarifa kuu

Rais wa Kenya William Ruto anazuru Rwanda

Nairobi – Rais wa Kenya William Ruto amewasili nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wake ,Rais Paul Kagame .Miongoni mwa agenda kuu za mazungumzo yao ikiwa ni biashara ya kikanda, usalama na hali ya chakula katika Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Rais wa Kenya William Ruto akutana na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame jijini Kigali
Rais wa Kenya William Ruto akutana na mwenyeji wake wa Rwanda Paul Kagame jijini Kigali © Statehouse Kenya
Matangazo ya kibiashara

Rwanda na Kenya zinasema mchango wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutuma jeshi lake Mashariki mwa DRC na kuongoza mchakato wa mazungumzo, unazaa matunda kufuatia kutoripotiwa kwa mapigano kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita. 

Rais Paul Kagame na mgeni wake William Ruto, wamesema wanamanini kuwa suluhu ya kudumu itapatikana. Huyu hapa ni rais Kagame. 

"Tunaona hatua inapigwa licha ya kuendela kuwepo kwa changamoto mbalimbali lakini tunapaswa kuendela kupiga hatua hii ili tupate suluhu  la amani ya kudumu."amesema Rais Paul Kagame.
00:37

PAUL KAGAME APRIL 04 2023 JIONI

Rais Ruto akizungumzia hali ya kisiasa nchini mwake baada ya Jumapili iliyopita, kutangaza mazungumzo na upînzani, amefafanua kuwa, hatua yake haimaniishi kuwa upinzani utajumuishwa kwenye serikali. 

"Hakutakua na handisheki ,lakini mazungumzo na mashauriano bungeni kuhusu masuala yanayoangaziwa na upianzani ili kuona ni yepi bunge linaweza kutatua."amesema Rais wa Kenya William Ruto .
00:39

WILLIAM RUTO APRIL 04 2023

Rais huyo wa Kenya anazuru Kigali kwa siku mbili, ambapo nchi hizo zimetiliana mikataba katika masuala ya elimu, afya na kilimo. 

Wachambuzi wa masula ya mambo wanahisi kuwa ziara hii huenda ikawa ya manufaa zaidi kwa nchi hizo mbili haswa katika masuala ya miundombinu kando na elimu na afya. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.