Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Kiongozi wa Hamas mjini Cairo kuzungumza usitishwaji vita

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh amewasili Cairo siku ya Jumanne ili kujadili kuhusu makubaliano mapya kuhusu usitishwaji vita huko Gaza, kundi la wanamgambo la Hamas limesema, katikati ya shinikizo la kimataifa la kusitishwa vita kati ya Israel na Hamas.

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh akisalimiana na waandishi wa habari alipowasili kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah Septemba 19, 2017.
Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh akisalimiana na waandishi wa habari alipowasili kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah Septemba 19, 2017. AFP/Said Khatib
Matangazo ya kibiashara

 

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, yenye makao yake makuu nchini Qatar, "atajadiliana na maafisa wa Misri kuhusu hali ya kisiasa na katika uwanja wa vita", Hamas inabainisha katika taarifa. Hamas iliyoko madarakani katika Ukanda wa Gaza unaokabiliwa na mashambulizi ya Israel tangu shambulio kundi hili kutekeleza shambulio baya ambalo halijawahi kutokea nchini Israeli mnamo Oktoba 7.

Bw. Haniyeh na ujumbe wake wanakusudia kutoa maoni yao kuhusu mpango uliowasilishwa wakati wa mkutano mwishoni mwa juma lililopita mjini Paris kati ya Mkurugenzi wa CIA William Burns na maafisa wa Misri, Israel na Qatar.

Kwa mujibu wa chanzo cha Hamas, kundi hilo linachunguza pendekezo katika awamu tatu, ya kwanza ikihusu usitishaji mapigano wa wiki sita ambapo Israel italazimika kuwaachia huru wafungwa 200 hadi 300 wa Kipalestina badala ya mateka 35 hadi 40 wanaoshikiliwa huko Gaza, na Malori 200 hadi 300 ya misaada yataweza kuingia katika ardhi ya Palestina kila siku.

Baada ya zaidi ya miezi minne ya vita, wakazi wa Gaza "wanakufa kwa njaa", Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya.

Wiki hii Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kwamba matakwa ya Hamas ni "udanganyifu." Ili kuunga mkono juhudi za uwezekano wa kupatikana kwa makubaliano ya pili, mkuu wa diplomasia ya Marekani, Antony Blinken, atarejea "katika siku zijazo" katika Mashariki ya Kati, amesema afisa wa Marekani bila kutaja nchi atakazozuru.

Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, makubaliano ya kwanza ya usitishwaji mapigano ya wiki moja yaliwezesha kuongezeka kwa msaada huko Gaza, kuachiliwa kwa matekazaidi ya mia moja kati ya takriban 250 waliotekwa nyara nchini Israeli mnamo Oktoba 7 na kupelekwa Gaza, na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina. Kulingana na Israel, mateka 130 bado wanazuiliwa huko Gaza, 30 kati yao wanaaminika kuwa walifariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.