Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Israel mjini Cairo kwa mazungumzo kuhusu makubaliano

Ujumbe wa Israel unaelekea Cairo siku ya Jumanne kwa mazungumzo mapya na maafisa wa Marekani, Qatar na Misri kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza ikiwa ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wa Israel na Hamas, kwa mujibu wa maafisa wa Israel. 

Mwanamke wa Kipalestina akiwa amemshika binti yake aliyejeruhiwa walipokuwa wakipanda mkokoteni unaovutwa na punda kuelekea kliniki huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 12, 2024.
Mwanamke wa Kipalestina akiwa amemshika binti yake aliyejeruhiwa walipokuwa wakipanda mkokoteni unaovutwa na punda kuelekea kliniki huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 12, 2024. © Mohammed Abed / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mkuu wa Mossad (Idara ya kijasusi ya Israeli katika nchi za kigeni), David Barnea, na mkuu wa Shin Bet (Idara ya usalama wa ndani), Ronen Bar, watakutana huko Cairo hasa na mkurugenzi wa CIA, shirika kuu la kijasusi la Marekani, Richard Burns, maafisa hao wameongeza kwa sharti la kutotajwa majina. 

Wataungana na Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdelrahman Al-Thani, pia mkuu wa diplomasia wa Qatar na mpatanishi wa mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano huko Gaza hapo awali. Hakuna wajumbe wa Hamas ambao wamepanga katika hatua hii kwenda Cairo kushiriki katika mijadala hii isiyo ya moja kwa moja inayofadhiliwa na Qatar na Misri, shirika la habari la AFP limeripoti likinukuu afisaa moja wa kundi la wanamgambo la Hamas siku ya Jumanne asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.