Pata taarifa kuu

Misri yajenga eneo salama kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao kutoka Gaza

Misri inajenga kambi iliyofungwa na salama katika eneo la Sinai ili kuwahifadhi Wapalestina kutoka Gaza wanaokimbia vita, katika tukio la mashambulizi ya Israel huko Rafah, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani na shirika lisilo la kiserikali la Misri.

Mpaka kati ya Gaza na Misri, kwa sasa umefungwa kwa kiasi kikubwa.
Mpaka kati ya Gaza na Misri, kwa sasa umefungwa kwa kiasi kikubwa. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Gazeti la Wall Street Journal linadai, likiwanukuu maafisa wa Misri na wataalam wa usalama, kwamba "kizimba kilichofungwa cha kilomita 13" kinajengwa kwenye mpaka na eneo la Palestina lililoharibiwa na zaidi ya miezi minne ya vita kati ya Israel na Hamas.

Kwa hivyo kambi hii ni sehemu ya "mipango ya dharura" ya kuwapokea wakimbizi hao, baada ya tangazo la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu mashambulizi ya kijeshi yanayokuja huko Rafah, na inaweza kuwahifadhi "zaidi ya watu 100,000", kulingana na gazeti la kila siku la Marekani.

Tangu kuanza kwa vita, Cairo imeonya dhidi ya "kuhama kwa nguvu" kwa wakazi wa Palestina kuelekea Sinai, wakati watu milioni 1.4, wengi wao wamekimbia mapigano, wanajaa katika mji huu unaokaribiana na mpaka uliofungwa na Misri.

Viongozi wa Palestina, Umoja wa Mataifa na nchi nyingi wameelezea wasiwasi wao kutokana na athari mbaya kwa wakazi kufuatia mashambulizi hayo, na kulaani kuundwa kwa kizazi kipya cha wakimbizi wasio na matarajio ya kurudi.

"Katika tukio la msafara wa watu wengi"

Katika ripoti iliyotolewa wiki hii, Wakfu wa Sinai wa Haki za Kibinadamu unasema Misri inajenga "eneo lililofungwa, lenye ulinzi mkali na lililotengwa" kwa ajili ya wakimbizi wa Kipalestina "katika tukio la kuhama kwa wingi."

Gavana wa Sinai Kaskazini, Mohamed Abdel Fadil Choucha, amekanusha ujenzi wowote wa aina hii lakini shirika lisilo la kiserikali la Misri limesisitiza kuwa viongozi wawili wa wafanyabiashara wa eneo hilo wamelithibitishia kwamba wamepata kandarasi za kujenga eneo lililofungwa "lililozungukwa na kuta za urefu wa mita saba.

Picha za satelaiti zilizopigwa siku ya Alhamisi na kuchunguzwa na shirika la habari la AFP zinaonyesha vifaa vya ujenzi vinavyojenga ukuta katika sehemu ya Rafah nchini Misri, eneo ambalo ni salama kabisa ambalo limefungwa kwa vyombo vya habari kutokana na operesheni za kijeshi dhidi ya wanajihadi. Ardhi hiyo pia ilisawazishwa, kulingana na picha zilizopigwa kati ya Februari 10 na 15.

Vita hivyo vilichochewa na shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7 kusini mwa Israel, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,160, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP klikinukuu data rasmi za Israeli.

Katika kulipiza kisasi, Israel ilianzisha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza ambayo yamesababisha vifo vya watu 28,775, wengi wao wakiwa raia, kulingana na ripoti ya hivi punde Ijumaa kutoka Wizara ya Afya ya Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.