Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Hamas watarajiwa mjini Cairo kujadili mpango wa kusitisha mapigano

Ujumbe wa Hamas unatarajiwa mjini Cairo siku ya Ijumaa kujadili mpango wa hatua tatu wa Misri unaotoa mapatano ya usitishwaji wa mapigano yanayoweza kurejelewa upya, kuachiliwa huru kwa mateka wa Kipalestina na wafungwa na, hatimaye, kusitisha mapigano kwa minajili ya kumaliza uhasama.

Muonekano wa angani wa Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, baada ya mashambulizi ya Israel, Desemba 26, 2023.
Muonekano wa angani wa Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, baada ya mashambulizi ya Israel, Desemba 26, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mjini Cairo, ujumbe wa Hamas utawasilisha kwa Misri "majibu ya makundi ya Wapalestina, ambayo yanajumuisha uchunguzi kadhaa, kwa mpango wao",  afisa wa Hamas ambaye hakutaka kutajwa jina ameliamia shirika la habari la AFP.

Maoni haya yanahusiana hasa "na utaratibu wa mabadilishano yaliyopangwa na idadi ya wafungwa wa Kipalestina ambao wataachiliwa, na kupata dhamana ya uondoaji kamili wa jeshi la Israeli kutoka Ukanda wa Gaza", ameongeza afisa huyu. “Tunawasiliana na wapatanishi tunapozungumza. Siwezi kutoa maelezo zaidi. Tunafanya kazi ya kuwarudisha wote,” alisema Waziri Mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu wakati wa mkutano Alhamisi mjini Tel Aviv na familia za mateka.

Wakati huo huo jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake kusini mwa Ukanda wa Gaza Ijumaa hii, Desemba 29.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.