Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Kiongozi wa Hamas awasili Misri kwa mazungumzo kuhusu usitishwaji vita

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh amewasili Cairo siku ya Jumatano kwa ajili ya majadiliano kuhusu hali ya Gaza, kundi hili la wanamgambo wa Kiislamu limesema huku Hamas na Israel zikiongeza ishara za kuunga mkono mapatano mapya ya usitishwaji vita. 

Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh na Mkuu wa Hamas katika Gaza Yehya Al-Sinwar wakionyesha ishara kwa wafuasi wao wakati wa mkutano wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Hamas, katika Jiji la Gaza Desemba 14, 2017.
Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh na Mkuu wa Hamas katika Gaza Yehya Al-Sinwar wakionyesha ishara kwa wafuasi wao wakati wa mkutano wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Hamas, katika Jiji la Gaza Desemba 14, 2017. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Akiwa nchini Qatar, Bw. Haniyeh amewasili "katika mji mkuu wa Misri kwa ajili ya majadiliano na maafisa wa Misri juu ya maendeleo ya uvamizi wa Wazayuni (Israeli) kwenye Ukanda wa Gaza na masuala mengine mengi," Hamas imesema katika taarifa yake.

Mazungumzo makali yanaendelea kwa ajili ya makubaliano ya pili ya usitishwaji vita

Mazungumzo makali yanaendelea kuhusu mapatano mapya huko Gaza, kulingana na chanzo kilicho karibu na suala hilo, linaripoti shirika la habari la REUTERS. Mazungumzo hayo chini ya upatanishi wa Qatar na Misri yanalenga kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wa Hamas ili kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina. Hamas imetangaza kuwa kiongozi wake aliye uhamishoni nchini Qatar, Ismaël Haniyeh, aliwasili Jumatano asubuhi mjini Cairo kukutana na mamlaka ya Misri, huku Rais wa Israel Isaac Herzog akihakikisha Jumanne kwamba nchi yake iko tayari kuhitimisha mapatano iwapo Hamas itakubaliana na hili.

Kwa mujibu wa chanzo kinachofahamu mazungumzo hayo, idadi ya mateka wanaotarajiwa kuachiliwa bado haijaamuliwa, lakini Israel inasisitiza kuwa wanawake na wanaume walio na afya mbaya wajumuishwe kwenye orodha hiyo. Kwa kubadilishana, Wapalestina waliofungwa nchini Israel kwa uhalifu mkubwa wanaweza kuachiliwa, kimeongeza chanzo hiki

Malaysia yapiga marufuku meli za mizigo za Israel kutia nanga kwenye bandari zake

Malaysia siku ya Jumatano imepiga marufuku meli za mizigo zenye bendera ya Israel kutia nanga kwenye bandari za nchi hiyo, kujibu operesheni za kijeshi huko Gaza, ambazo Kuala Lumpur inasema "zinapuuza kanuni za kimsingi za kibinadamu." Meli zinazoelekea Israel pia zitapigwa marufuku kupakia bidhaa katika bandari yoyote katika nchi hii ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye Waislamu wengi, Waziri Mkuu wake, Anwar Ibrahim, amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.