Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza: Uturuki inamuomba Blinken kusitisha mapigano 'mara moja'

Mapigano makali yanaendelea kurindima kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo jeshi la Israel linadai kugawanya ukanda wa Gaza sehemu mbili, na kukataa kuitikia wito unaozidi kuongezeka wa kusitishwa mapigano na katikati ya ziara ya kikanda ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken inayolenga kushawishi nchi mbalimbali kutoa misaada ya kibinadamu. 

Katika Hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 6, 2023.
Katika Hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 6, 2023. AFP - BASHAR TALEB
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio haya ya mabomu yanawakumba raia hasa, ikiwa ni pamoja na kusini mwa eneo hilo. Takriban Wapalestina milioni 2.4 wamezingirwa na kunyimwa maji, chakula na umeme tangu Oktoba 9.

Unachopaswa kufahamu:

► Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anamwomba Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuitaka Israel kusitisha mapigano "mara moja" na "kamili" katika Ukanda wa Gaza.

► Jeshi la Israeli lilifanya "mashambulio makubwa" usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu. Kulingana na jeshi, wataendelea na mashambulizi katika siku zijazo huko Gaza, eneo ambalo sasa limegawanywa mara mbili ikia ni pamoja na "Gaza Kusini na Gaza Kaskazini". Wizara ya Afya ya Hamas imetangaza vifo zaidi ya 200 katika mashambulizi haya ya anga ya usiku.

► Mfalme Abdullah II wa Jordan ametangaza kuwa vifaa mbalimbali vilidondoshwa kwa ndege, mapema Jumatatu, Novemba 6, kama sehemu ya msaada wa dharura wa matibabu kwa Gaza, msaada ambao umekusudiwa kwa hospitali ya Jordan inayowahudia raia wa Gaza.

► Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken alikutana na Mahmoud Abbas siku ya Jumapili. Rais wa Mamlaka ya Palestina alishutumu "mauaji ya halaiki" katika Ukanda wa Gaza na Israel.

► Tangu Oktoba 7, zaidi ya Waisraeli 1,400 wameuawa, wakiwemo wanajeshi 341, na jeshi la Israel linaripoti watu 240 wanaoshikiliwa mateka na Hamas. Wizara ya Afya ya Hamas imetangaza idadi ya vifo vya Wapalestina 9,770, wakiwemo watoto 4,800.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.