Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anazuru Ankara Uturuki

Nairobi – Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, yuko mjini Ankara Uturuki, ambako amefanya mazungumzo na wenyeji wake, yanayolenga kujaribu kutuliza joto baina ya mshirika huyo wa karibu na utawala wa Washington, hasa kuhusu vita kati ya Israel na Hamas.

Kwa muda sasa Uturuki, kama mataifa mengine ya Kiislamu, yameendelea kuikashifu Israel na hata kumuita nyumbani balozi wake
Kwa muda sasa Uturuki, kama mataifa mengine ya Kiislamu, yameendelea kuikashifu Israel na hata kumuita nyumbani balozi wake REUTERS - ELIZABETH FRANTZ
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda sasa Uturuki, kama mataifa mengine ya Kiislamu, yameendelea kuikashifu Israel na hata kumuita nyumbani balozi wake, ziara ya Blinken ikijaribu kutoa hakikisho kwa Ankara kuhusu eneo la mashariki ya kati.

“Ukiangalia mustakabali ujao kile sote tunakubaliana kuhusu tafsiri ya huo mustakabali wa Gaza na Ukingo wa Magharibi na mwisho taifa la Palestina ni kwamba sauti za raia wa Palestina lazima ziwe kiini cha suluhu.” alisema Antony Blinken.

00:29

Antony Blinken kuhusu Gaza

Ziara ya Blinken nchini Uturuki, imekuja saa chache tangu atembelee ukingo wa magharibi ambako alikutana na rais Mahmud Abbas, kabla ya kufanya ziara ya ghafla nchini Iraq.

Blinken pia alizuru ukingo wa magharibi ambako alikutana na rais Mahmud Abbas
Blinken pia alizuru ukingo wa magharibi ambako alikutana na rais Mahmud Abbas AFP - JONATHAN ERNST

Tayari waziri waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa shinikizo la Antony Blinken kusitisha vita vyake dhidi ya Hamas ilikuruhusu misaada ya kibinadam, akiweka masharti ya kuachiliwa kwa mateka waliochukuliwa kutoka Israel hadi Gaza.

Haya yanajiri wakati huu taasisi ya Ufaransa huko Gaza ikiathiriwa na shambulio la anga la Israel, lakini hakuna majeraha yaliyoripotiwa kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa.

Israel inasema inawasaka wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza ikiaapa kutokomeza kundi hilo kabisa
Israel inasema inawasaka wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza ikiaapa kutokomeza kundi hilo kabisa via REUTERS - POOL

Ufaransa imezitaka mamlaka za Israel kueleza sababu za shambulio hilo dhidi ya taasisi hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Catherine Colonna katika taarifa yake amesema raia 34 wa Ufaransa na familia zao walivuka hadi Misri kutoka Gaza kupitia mpaka wa Rafah siku ya Ijumaa.

Rais Emmanuel Macron aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake huko Brittany kwamba Ufaransa inaanza kuwahamisha raia wake, Macron akisisitiza wito wake wa kusitisha mapigano ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.