Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Rais wa Iran Ebrahim Raisi aonyesha azma yake dhidi ya waandamanaji

Siku moja baada ya kunyongwa kwa Mohsen Shekari, aliyepatikana na hatia ya kumshambulia afisa wa vikosi vya usalama na kujaribu kuzuia shughuli  mbalimbali mwanzoni mwa maandamano, mamlaka za Iran zimeongeza haua kali dhidi ya waandamanaji.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi mnamo Septemba 2022.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi mnamo Septemba 2022. AP - Vahid Salemi
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na familia za maafisa wa vikosi vya usalama waliouawa katika miezi ya hivi karibuni, Rais Raisi amethibitisha kwamba mamlaka "itatenda kwa dhamira ya kuwatambua, kujaribu na kuwaadhibu wahalifu", neno linalotumiwa na mamlaka kubaini wale waliofanya vitendo vya ukatili wakati wa maandamano ya miezi mitatu iliyopita.

Kauli ya Rais wa Iran imekuja wakati nchi nyingi za Magharibi zikilaani kunyongwa kwa Mohsen Shekari na licha ya mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini ni wazi, mamlaka imeamua kupaza sauti ili kujaribu kukomesha maandamano. Akiunga mkutno uamuzi wa serikali, Ayatollah Ahmad Khatami, kongozi mkuu wa kidini wa Iran, amepongeza mahakama kwa uamuzi wake wa "kumuweka kitanzi" Mohsen Shakeri, kulingana na maneno aliyotumia.

Katika hali hizi, kunahofiwa watu wengine kunongwa katika siku zijazo. Kwa hakika, mkuu wa idara ya mahakama alithibitisha Jumapili iliyopita kwamba hukumu ya kifo ya watu kadhaa imethibitishwa na Mahakama ya Juu na itatumika hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.