Pata taarifa kuu

Jordan: Watu kumi na wanne wamekufa baada yakuporomoka kwa jengo Amman

Idadi ya vifo kutokana na kuporomoka kwa jengo la makazi katika mji mkuu wa Jordan imeongezeka hadi 14, msemaji wa usalama wa umma amesema Jumamosi (Septemba 17), akiongeza kuwa shughuli za utafutaji na uokoaji zimekamilika.

Jengo hili la ghorofa nne liliporomoka katika wilaya ya Jabal Al-Weibdeh, miongoni mwa jengo kongwe zaidi mjini Amman, mji mkuu wa Jordan (kwenye picha).
Jengo hili la ghorofa nne liliporomoka katika wilaya ya Jabal Al-Weibdeh, miongoni mwa jengo kongwe zaidi mjini Amman, mji mkuu wa Jordan (kwenye picha). Getty Images/Valery Sharifulin/Contributeur
Matangazo ya kibiashara

"Timu za uokoaji zimeweza kumtoa mtu mmoja aliyefariki Jumamosi, idadi ya waliofariki sasa imefikia 14," Amer Al-Sartawi, msemaji wa usalama wa umma, amesema katika taarifa. Idadi ya hapo awali iliripoti kuwa watu 13 walikufa.

Bw Sartawi ameongeza kuwa wote walionasa chini ya vifusi wamepatikana, wakiwa hai au wamekufa, na hivyo kusababisha kumalizika kwa shughuli za kuwatafuta.

Kulingana na chanzo cha Hospitali, mwathiriwa wa mwisho aliyegunduliwa ni mwanamke, na maiti ya binti zake wawili ilikuwa imetolewa katika siku za hivi karibuni.

Jengo hili la ghorofa nne liliporomoka katika wilaya ya Jabal Al-Weibdeh, miongoni mwa jengo kongwe zaidi mjini Amman.

Vikosi vya uokoaji viliweza kuwatoa manusura wawili saa 24 baada ya mkasa huo: mtoto wa miezi minne na mwanamume mwenye umri wa miaka 45, kulingana na usalama wa umma.

Mamia ya maafisa wa kikosi cha ulinzi wa raia walishiriki katika msako huo, kulingana na mkurugenzi wa kikosi cha ulinzi wa raia Hatem Jaber.

Upande wa mashtaka uliamuru kukamatwa kwa watu watatu ikiwa ni sehemu ya uchunguzi, akiwemo meneja wa jengo hilo pamoja na watu wengine wawili waliohusika katika shughuli za ukarabati zinazodaiwa kufanywa kwenye jengo hilo, kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Petra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.