Pata taarifa kuu

Nyuklia ya Iran: Washington yamtaka rais Raïssi kufanya mazungumzo

Marekani imemtaka rais mpya wa Iran Ebrahim Raïssi kuanza tena mazungumzo juu yakurejea kwa Washington na Tehran kwenye makubaliano ya mwaka 2015 juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, akibaini kwamba dirisha la kidiplomasia halitabaki wazi kwa muda usiojulikana.

Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raissi.
Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raissi. AP - Vahid Salemi
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na Ebrahim Raïssi kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi, taasisi zote za serikali sasa zinadhibitiwa na wafuasi wenye itikadi kali dhidi ya Magharibi, kulingana na msimamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu , Ayatollah Ali Khamenei.

Mazungumzo ya moja kwa moja yaliyofanywa mwaka huu katika mji mkuu wa Austria Vienna kati ya Marekani na Iran yalisitishwa mwezi Juni, baada ya vikao kadhaa vya mazungumzo, sambamba na kufanyika kwa uchaguzi wa urais wa Iran.

"Ujumbe wetu kwa rais Raïssi ni sawa na ule tulioutoa kwa watangulizi wake (...) Marekani itatetea na kuendeleza masilahi yake na ya washirika wake katika maswala ya usalama wa kitaifa", amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.