Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-USALAMA-NDEGE

Ndege ya kivita ya Marekani yaangushwa na Iran

Ndege ya kijeshi ya Marekani isiyokuwa na rubani, imeangushwa na kombora kutoka jeshi la Iran, katika angaa la Kimataifa la Strait of Hormuz katika eneo guba ya Oman.

Ndege ya kivita ya Marekani
Ndege ya kivita ya Marekani US NAVY/KELLY SCHINDLER
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Marekani limethibitisha hilo na kusema kuwa ndege iliyoangushwa ni aina ya MQ-4C Triton.

Jeshi la Iran awali lilithibitisha kuangusha ndege hiyo ambayo ilikuwa inapaa katika angaa lake karibu na eneo la Kuhmobarak karibu na mkoa wa Hormozgan.

Tukio hili linakuja wakati huu wasiwasi ukiendelea kushuhudiwa kati ya Marekani na Iran.

Siku ya Jumatatu, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza kuwa ilikuwa inatuma wanajeshi zaidi ya 1,000 katika eneo la Mashariki ya Kati, kwa kile inachosema kuwa ni kukabiliana na tabia mbaya ya jeshi la Iran.

Iran imetishia kuendelea na urutubishaji wa Uranium licha ya mkataba wa Kimataifa uliotiwa saini mwaka 2015, wakati huu Marekani ikiendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.