Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI

Marekani yaituhumu Iran kuhusika na mashambulizi ya meli za mafuta

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameilaumu nchi ya Iran kwa kile alichosema mashambulizi dhidi ya meli za mafuta kwenye pwani ya nchi za Ghuba.

Meli ya mafuta ikionekana ikiwaka moto kwenye bahari ya ghuba ya Oman baada ya kushambuliwa, June 13, 2019.
Meli ya mafuta ikionekana ikiwaka moto kwenye bahari ya ghuba ya Oman baada ya kushambuliwa, June 13, 2019. ©ISNA/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS -
Matangazo ya kibiashara

Pompeo amesema nchi yake imefanya tathmini kwa kutumia intelijensia yake kuhusu aina ya silaha iliyotumika.

Awali afisa mmoja wa juu katika Serikali ya Iran alikanusha nchi yake kuwa na mkono katika mashambulizi ya hivi karibuni kama ambavyo Marekani inadai.

Mamia ya wafanyakazi waliokolewa baada ya kutokea mlipuko katika meli moja ya Japan na meli nyingine ya Norway.

Pande zote mbili, Iran na Marekani zimesema ziliwaokoa wafanyakazi hao.

Mlipuko huu umetokea katika moja ya njia kuu ya meli za mafuta, na ni tukio linalotokea baada ya mwezi mmoja tu kupita tangu kutokea kw tukio kama hili ambapo meli ya falme za kiarabu ilishambuliwa.

Hakuna kundi wala nchi iliyokiri kuhusika kwenye tukio la mwezi Mei na hakuna aliyejeruhiwa.

Katika tukio la mwezi uliopita Marekani ilidai tena kuwa Iran ndio ilihusika kujaribu kutengeneza mzozo kwenye nchi za mashariki ya kati.

Bei ya mafuta katika soko la dunia ilipanda kwa karibu asilimia 4.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.