Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-AFRIKA KUSINI-USALAMA

Machafuko Gaza: Afrika Kusini yamrejesha nyumbani balozi wake Israeli

Afrika Kusini imechukua uamuzi wa kumrejesha nyumbani balozi wake nchini Israeli baada ya vifo vya Wapalestina zaidi ya 50 Jumatatu Mei 14 katika ukanda wa Gaza, ikiwa ni pamoja na watoto 8, na zaidi ya 2,400 kujeruhiwa na jeshi la Israel.

Machafuko yaliyoukumba Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na wengine wengi kujeruhiwa, Mei 14, 2018.
Machafuko yaliyoukumba Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na wengine wengi kujeruhiwa, Mei 14, 2018. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili baya lilitokea kwenye mpaka kati ya Ukanda wa Gaza na Israel, siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 70 ya taifa la Kiyahudi na siku ya ufunguzi rasmi wa ubalozi wa Marekani Jerusalem.

Uzinduzi huo ulikaribishwa kama wa kihistoria na Israeli, lakini kwa nchi nyingi ziliona kuwa ni kitendo cha uchokozi, kwa sababu inakuja kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Kiyahudi. Nchi nyingi zilikataa mwaliko wa kuhudhuria uzinduzi huo wa ubalozi mpya wa Marekani.

Afrika Kusini imekua nchi ya kwanza katika bara la Afrika kulaani na kushtumu machafuko hayo. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu jioni, serikali ya Afrika Kusini ilibaini kwamba kutokana na tabia mbaya na ya kikatili ya shambulio la Israeli, Pretoria inamrejesha nyumbani balozi wake, huku taarifa hiyo ikiongeza kuwa uzinduzi wa Ubalozi wa Marekani Jerusalem ni kitendo cha uchochezi.

Afrika Kusini imekuwa ikiunga mkono Wapalestina, ambapo inaona kuwa mapambano yao yamekaribiana na yale ya wafuasi wa ANC wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi. Mnamo mwezi Desemba mwaka uliyopita, wakati Umj awa Mataifa ulipiga kura ya kulaani hatua ya Marekani ya kutambuwa Jerusalemu kama mji mkuu wa Israeli, nchi nyingi za Kiafrika zilijumuisha kura zao kwa kulaani hatua hiyo.

Togo ndiyo nchi pekee ya Afrika iliunga mkono Marekani. Nchi nyingine nane zilijizuia, hasa washirika wa Marekani ikiwa ni pamoja na Sudan Kusini, Rwanda na Uganda.

Wakati huo Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kufunga msaada wa fedha kwa nchi zilizojaribu kushtumu uamuzi wa Marekani, akizituhumu "wale wanaotumia fedha zetu na kisha wanapiga kura dhidi yetu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.