Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-UGAIDI

Vikosi vya Syria vyadhibiti asilimia 10 ya ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta

Wanajeshi wa Syria wamefanikiwa kuchukua asilimia 10 ya ngome ya wapiganaji wa upinzani Mashariki mwa Ghouta, jijini Damacus.

Uharibifu uliotokea Mashariki mwa  Ghouta, jijini Damascus nchini Syria
Uharibifu uliotokea Mashariki mwa Ghouta, jijini Damascus nchini Syria REUTERS/Bassam Khabieh.
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi na watetezi wa Haki za binadamu nchini Syria wanasema kuwa mapigano yamekuwa yakishuhudiwa katika ngome hiyo ya upinzani kuanzia siku ya Jumamosi.

Mapigano haya yamesabisha waathiriwa wa vita hivi ambao ni raia wa kawaida zaidi ya laki tatu kushindwa kupata misaada ya kibinadamu.

Hii ndio ngome pekee ya upinzani inayosalia jijini Damascus katika vita dhidi ya rais Bashar Al Assad.

Watu zaidi ya 600 wamepoteza maisha katika ngome hiyo ya upinzani ndani ya wiki nne zilizopita.

Syria imekataa kutekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha vita kwa siku 30 ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa.

Hata hivyo, Urusi imesema vita vinasitishwa kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana kuwaruhusu raia wa kawaida kuondoka katika ngome hiyo ya upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.