Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-SYRIA

Marekani yashtumu Urusi na Syria kukiuka azimio la UN

Marekani imeishtumu Urusi na serikali ya Syria kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano Mashariki mwa Ghouta, licha ya kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Raia wanaendelea kuyatoroka makazi yao kufuatia mashambulizi mashariki mwa Ghouta.
Raia wanaendelea kuyatoroka makazi yao kufuatia mashambulizi mashariki mwa Ghouta. REUTERS/ Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Marekani inasema mapigano yanayoendelea kushuhudiwa katika ngome hiyo ya upinzani, ni ishara tosha kuwa azimio hilo lililopitishwa Jumamosi iliyopita,halijaheshimiwa.

Ilikubaliwa kuwa, vita vingesitishwa kwa muda wa siku 30 katika ngome hiyo ya upinzani ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa wa vita vinavyoendelea.

Urusi ambayo inasaidia Syria, imeamua kuwa vita usitishwaji wa mapigano utadumu kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana, ili kuwaruhusu raia wa kawaida kuondoka katika ngome hiyo ya upinzani.

Kauli hii ya Marekani imekuja wakati huu mashirika ya kutetea haki za binadamu yakisema kuwa raia wa kawaida 600 waliuawa mwezi Februari katika ngome ya upinzani ya Ghouta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.