Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI

Marekani yailaumu Urusi kwa shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria

Marekani imeishutumu Urusi kwa kushindwa kuizuia serikali ya Syria kutekeleza shambulizi la  silaha za kemikali na kusababisha vifo vya watu 87 katika mkoa wa Idlib ,lakini mataifa hayo mawili yamekubaliana kuharibu silaha za kemikali za Syria.

Madaktari wakimhudumia mwathirika wa shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria
Madaktari wakimhudumia mwathirika wa shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria Ziv medical center
Matangazo ya kibiashara

Wakati uo huo, Marekani inasema amani ya kudumu haiwezi kupatikana nchini Syria, ikiwa rais Bashar Al Assad ataendelea kusalia madarakani.

Waziri wa Mambo ya nje Rex Tillerson ametoa kauli hiyo na kuongeza kuwa mshirika wa Syria ambaye ni Urusi, ihakikishe kuwa silaha za kemikali hazitumiwi tena kuwashambulia raia wa Syria.

Aidha, amesema ikiwa Urusi haitazuia mashambulizi mengine basi, uhusiano kati ya Washington DC na Moscow utakuwa mbaya zaidi.

Tillerson anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov siku ya Jumanne kuzungumzia shambulizi la wiki iliyopita.

Urusi imelaani hatua ya Marekani kushambulia uwanja wa kijeshi wa Syria wiki iliyopita na kuharibu silaha zake za kivita, baada ya kuaminiwa kuwa uwanja huo ndio uliotumiwa kutekeleza shambulizi hilo.

Rais Donald Trump, alisema aliagiza kushambuliwa kwa Syria kutokana na sera yake ya usalama na kuzingatia usalama wa nchi yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.