Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA

Marekani yatekeleza shambulizi katika uwanja wa ndege wa kijeshi nchini Syria

Marekani imetekeleza shambulizi katika uwanja wa ndege wa kijeshi nchini Syria, eneo ambalo linaaminiwa kuwa serikali ya Syria ilirushia silaha za kemikali kwenda katika mkoa wa Idlib wiki hii na kusababisha vifo vya watu 86 wakiwemo watoto 27 na kuwajeruhi wengine 500.

Shambulizi la Marekani katika uwanja wa ndege wa kijeshi April 7 2017
Shambulizi la Marekani katika uwanja wa ndege wa kijeshi April 7 2017 cdn.com
Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amesema ameagiza kutekelezwa kwa shambulizi hilo baada ya kubainika kuwa serikali ya Syria ndio iliyohusika na kukiuka sheria za Kimataifa, zinazouia matumizi ya silaha za kemikali .

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo limeharibu kabisa uwanja huo wa kijeshi na kuwauwa wanajeshi wanne wa Syria.

Trump ameyataka mataifa mengine duniani, kushirikiana pamoja na kumaliza mzozo wa Syria na kumwita Assad kama dikteta ambaye amewauawa watu wake.

Uingereza na Uturuki zimesema  zinaunga mkono shambulizi hili huku Iran ikilaani.

Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria, imedai kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na waasi wanaopambana na uongozi wa Damascus.

Rais Bashar Al Assad naye amesema kuwa, jeshi lake haliwezi kutumia silaha za kemikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.