Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-SYRIA

Marekani na Urusi bado sana kufikia makubaliano kuhusu mzozo wa Syria

Serikali ya Marekani imesema mpaka sasa hawajafikia hatua yoyote ya kukubaliana na nchi ya Urusi kuhusu kumaliza vita nchini Syria, ikiutuhumu utawala wa Moscow kwa kurejesha masuala ambayo ilidhani walishayamaliza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (Kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (Kulia) wakipeana mikoni wakati wa mazungumzo yao kuhusu Syria, mjini Geneva, Uswis, Agosti 26, 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry (Kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (Kulia) wakipeana mikoni wakati wa mazungumzo yao kuhusu Syria, mjini Geneva, Uswis, Agosti 26, 2016. REUTERS/Martial Trezzini/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, Barack Obama, amesema kuwa pande hizo mbili zinazungumza kwa kina kando na mkutano wa wakuu wa nchi za G20 wanaokutana nchini China, huku akisema kuwa suala lililoko mezani ni gumu sana kuafikiana.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa makubaliano yako karibu kufikiwa na huenda yakatangazwa na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo John Kerry sambamba na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, lakini baadae ikakiri kuwa mambo hayajawa vizuri.

Taarifs ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa, nchi ya Urusi imerejesha baadhi ya masuala ambayo walihisi waliyamaliza, na hivyo wamelazimika kurejea tena mazungumzo ya awali kabla ya kuendelea mbele kufikia muafaka.

Waziri Kerry na mwenzake wa Urusi, watakutana tena siku ya Jumatatu mjini Hangzhou, ambaki wakuu wa nchi za G20 wanakutana.

Utawala wa Moscow na Washington wote wanafadhili na kuunga mkono pande tofauti nchini Syria ambazo zinahusika kwenye mgogoro, ambao uliibuka mwezi Machi 2011 baada ya Rais Bashar al-Assad kutumia nguvu kukabiliana na waandamanaji waliokuwa wanapinga utawala wake.

Mazungumzo mfululizo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya kimataifa kujaribu kutuliza hali ya vita nchini Syria vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitano na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki 2 na elfu 90 na wengine mamilioni kulazimika kuikimbia nchi yao, yamekwama, huku maelfu wakikimbilia kuomba hifadhi barani Ulaya.

Nchi ya Urusi ni mmoja wa washirika wa karibu wa utawala wa Damascus, wakati Serikali ya Marekani yenyewe ikiwasaidia waasi wanaoipinga Serikali na wale wanaikabiliana na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.