Pata taarifa kuu
UN-SYRIA-IS

Mgawanyiko katika UN juu ya matumizi ya silaha za maangamizi na serikali ya Syria

Katika mji wa New York, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili Jumanne hii Agosti 30 ripoti juu ya matumizi ya silaha za maangamizi nchini Syria. Wataalam wote wanakubaliana kwamba Serikali ya Bashar al-Assad ilifanya makosa ya mashambulizi mawili ya chlorine kaskazini magharibi mwa nchi mwaka 2014 na 2015.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na kuchunguza matumizi ya silaha za maangamizii nchini Syria, Agosti 28, 2013, karibu na mji wa Damascus.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na kuchunguza matumizi ya silaha za maangamizii nchini Syria, Agosti 28, 2013, karibu na mji wa Damascus. REUTERS/Mohamed Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Kundi la Islamic State limenyooshewa kidole kuhusika na shambulio jingine kwa gesi ya haradali mwaka 2015. Serikali ya Syria inakanusha madai yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa na Shirika linalopiga marufuku silaha za kemikali, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litashindwa kuoa msimamo wa pamoja kutokana na hali hiyo. Hata hivyo Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Serikali ya Syria, huenda ikapinga azimio lolote la Barazala la Usalama la Umoja wa Mataifa. Itafahamika kwamba Urusi imeendelea kupinga Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu kushughulikia mauaji yaliyotekelezwa nchini Syria.

Ufaransa na Uingereza wamesema mauaji na vitendo vingine viovu vilivyotekelezwa nchini Syria ni "uhalifu wa kivita." Marekani imeonya kuwa serikali ya Syria "inapaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa mashambulizi haya." Lakini Urusi haikubaliani na madai hayo. Urusi , mshirika wa karibu wa Utawala wa Bashar al-Assad, imetangaza kuwa haijawa tayari kukubali hitimisho za ripoti hiyo.

Moscow ilisahihishwa azimio la kuanzishwa kwa uchunguzi mwaka mmoja uliopita, lakini balozi wake katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alibaini hata hivyo kwamba kulipatikana "silaha ya uhalifu, lakini hapakuwa na ushahidi juu ya hilo". Mwenzake wa Syria alibaini kwamba na hila za kisiasa, akisema hata hivyo kuwa hapakuwa na ushahidi wa matumizi ya klorini katika mashambulizi yote mawili ambapo serikali yake inaohusishwa.

Virginia Gamba, ambaye aliongoza uchunguzi, ameendelea kusisitiza kwamba alikuwa na taarifa za kutosha kwa kuzishtumu helikopta za serikali ya Syria, na amethibitishwa matumizi ya gesi ya haradali na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.