Pata taarifa kuu
SYRIA-IS

Syria: IS yavitimua vikosi vya serikali Raqa

Wanajihadi wa kundi la Islamic State (IS) walivitimua Jumatatu hii vikosi vya serikali ya Syria katika mkoa wa (kaskazini) baada ya kujihami mashambulizi ya jeshi la nchi hiyo yaliyosababisa vifo vya askari 40 wanaunga mkono serikali katika masaa 24, shirika lisilo la kiserikali limesema.

Vikosi vya serikali ya Syria vikipiga doria katika mji wa Khan Touman.Aprili 11, 2016.
Vikosi vya serikali ya Syria vikipiga doria katika mji wa Khan Touman.Aprili 11, 2016. George Ourfalian / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ilikua ilizindua Juni 3 mashambulizi kwa lengo la kuudhibiti mji muhimu wa Tabqa katika mkoa wa Raqa, ikisonga mbele kwa kilomita zaidi ya ishirini.

Lakini wanajihadi wamefaulu kuvitimua vikosi vya serikali hadi nje ya mkoa huo baada ya kujihami mashambulizi ya jeshi la serikali siku moja kabla, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu la Syria (OSDH).

"Kundi la Islamic State limefaulu kuvitimua vikosi vya serikali hadi nje ya mkoa wa raqa, baada ya kujihami mashambulizi ya jeshi yalizinduliwa Jumapili jioni," OSDH imesema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa shirika hilo lisilo la kiserikali, kundi la IS limewatuma mamia ya wapiganaji wake katika mji wa Raqa, mji mkuu wa kundi la wanajihadi hao Tabqa, kwa kuudhibiti mji huo ambao vikosi vya serikali vilikua vikilenga kuuteka.

Shirika hili, ambalo lina mitandao ya vyanzo nchini kote Syria, limesema kuwa "zaidi ya askari 40 wa vikosi vya serikali wameuawa" katika vita hivyo.

Mji wa Tabqa unapatikana kwenye umbali wa kilomita 50 magharibi wa mji wa Raqa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.