Pata taarifa kuu
UN-SYRIA-IS

UN yalaani mauaji yanayotekelezwa na IS Syria

Umoja wa Mataifa unasema wapiganaji wa Islamic State wanaendelea kuteketeleza mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Yazidi nchini Iraq na Syria.

Watu kutoka jamii ya Yazidi wakiyakimbia makazi yao kwa hofu ya kuuawa na kundi la Islamic State katika mji wa Sinjar.
Watu kutoka jamii ya Yazidi wakiyakimbia makazi yao kwa hofu ya kuuawa na kundi la Islamic State katika mji wa Sinjar. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Yazidi ni watu ambao sio Waislamu wala Waarabu na ni kundi dogo ya Wakiristo na watu wengine ambao wana imani tofauti mbali na Uislamu katika nchi hizo.

Mkuu wa Tume ya Umoja huo inayochunguza mauaji yanayoendelea nchini Syria Paulo Pinheiro, amesema kinachoendelea nchini Syria ni mauaji ya kimbari ambayo yanayendelea kushuhudiwa kila siku.

Ripoti ya Tume hiyo inaeleza kuwa, watu hao hukusanywa pamoja na kuuliwa, baada ya kuteswa mauaji ambayo yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2014.

Mbali na mauaji hayo, wasichana wadogo wenye umri wa miaka 9 na wanawake pia wameendelea kubakwa na kundi hilo.

Mbali na hilo, Urusi imetangaza usitishwaji wa vita katika mji wa Allepo kwa muda wa saa 48, hatua inayokuja baada ya Marekani kutangaza uvumilivu wake unafika mwisho kuhusu mapigano nchini Syria.

Uchunguzi unaonesha kuwa, utulivu umeanza kushuhudiwa katika mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.