Pata taarifa kuu
IRAQ-IS-MAPIGANO

Jeshi la Iraq latangaza kuukomboa mji wa Ramadi

Vikosi vya Iraq vimetangaza leo Jumatatu kwamba "vimeukomboa" mji wote wa Ramadi, ambao ni mji mkubwa magharibi mwa mji wa Baghdad, na kupandisha bendera ya taifa kwenye ya jengo kubwa la serikali kwa kuashiria ushindi wao mkuu dhidi ya kundi la Islamic State Group (IS).

Askari wa vikosi vya usalama wakipandisha bendera ya Iraq katika mji wa Ramadi.
Askari wa vikosi vya usalama wakipandisha bendera ya Iraq katika mji wa Ramadi. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Mji wa Ramadi umekombolewa", jenerali Yahya Rasool ametangaza kwenye runinga ya taifa.

Askari wamecheza wakipandisha silaha juu katika mitaa ya mji mkuu wa mkoa wa magharibi Al-Anbar, wakati ambapo maafisa waandamizi wamekua wakimiminika katika mji huo, ambo jeshi la Iraq lilikua lilipoteza tangu mwezi Mei.

Raia wa Iraq pia wameiingia mitaani ya miji mbalimbali nchini kote kusherehekea udhibiti wa mji wa Ramadi.

Wapiganaji wa kundi la Islamic State wanaweza kuwa bado wapo katika baadhi ya maeneo ya mji huo lakini vikosi vya Iraq vinasema hawajakutana na upinzani wowote tangu wapiganaji wa mwisho wa IS kuondoka Jumapili katika jengo kubwa la serikali, katikati mwa mji wa Ramadi.

Hata hivyo, wanajeshi wanasonga mbele kwa uangalifu, huku wakiwa na kazi kubwa ya kutegua mamia ya mabomu na vilipuzi vilivyoachwa na wapiganaji wa Islamic State katika mji huo.

- Vilipuzi 300 -

"Kuna mabomu na vilipuzi visiopungua 300 katika jengo la serikali na kwenye barabara inayoelekea kwenye jengo hilo", afisa wa bataliani ya 8 ya jeshi la Iraq, Majid al-Fatlawi ameeleza.

Karibu raia wote wameondoka katikati ya mji wa Ramadi unaokumbwa na mapigano. Baadhi wamehamishwa lakini wengine wamekuwa wakitumiwa kama ngao ya binadamu na wapiganaji wa kundi la IS ili waweze kuukimbia mji huo wakielekea mashariki ya mji, kwa mujibu wa mashahidi kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.