Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAQ-ISI-USALAMA

Iraq: Ikulu ya Marekani yatangaza kifo cha kiongozi namba mbili wa IS

Ikulu ya Marekani imetangaza kifo cha Hadji Moutazz, kiongozi namba mbili wa kundi la Islamic State. Inakisiwa kuwa Hadji Moutazz aliuawa Jumanne Agosti 18 katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani, karibu na mji wa Mosul nchini Iraq.

Hadji Moutazz alionekana mtu muhimu sana katika kundi la Islamic State mwezi Juni mwaka 2014, baada ya kundi hili kuudhibiti mji wa Mosul.
Hadji Moutazz alionekana mtu muhimu sana katika kundi la Islamic State mwezi Juni mwaka 2014, baada ya kundi hili kuudhibiti mji wa Mosul. AFP PHOTO / YOUTUBE
Matangazo ya kibiashara

" Fadhil Ahmad al-Hayali, ambaye pia anajulikana kwa jina la Hadji Moutazz, aliuawa katika mashambulizi ya jeshi la Marekani Agosti 18 wakati alipokua akitembea katika gari karibu na mji wa Mosul nchini Iraq, akiambatana na Abu Abdallah, afisa anaye husika na vyombo vya habari ", amesema msemaji wa Ikulu ya Marekani.

Hadji Moutazz alikua akiongoza Baraza la kieshi la kund la Islamic Statei tangu mwezi Juni mwaka 2014 baada ya kifo cha mtangulizi wake, Adnan Ismail al-Bilaoui, aliyeuawa katika mashambulizi ya jeshi la Marekani. Baraza hili, linaundwa na wajumbe kati ya 9 hadi 13, na ni taasisi kubwakatika uongozi wa kundi hili la Islammic State, ameeleza mwandishi wa RFI katika mji wa Beirut, Paul Khalifeh. Baraza hili linasimamia shughuli za kijeshi, linafafanua mikakati na kuamua vita na amani. Uratibu kati ya wakuu wa majimbo mbalimbali ya eneo linaloshikiliwa na Islamic State ni miongoni mwa majukumu ya mkuu wa Baraza hili la kijeshi.

Hadji Moutazz alikuwa akichukuliwa kama kiongozi namba mbili wa kundi la Islamic State. Jukumu lake lilikuwa muhimu zaidi hata kama alikua akielekeza shughuli za kijeshi za kundi hilo nchini Iraq. Alionekana mtu muhimu sana katika kundi la Islamic State mwezi Juni mwaka 2014, baada ya kundi hili kuudhibiti mji wa Mosul.

Hadji Moutazz ni raia wa Iraq. Kama washirika wengi wa karibu wa kiongozi mkuu wa kundi la Islamic State, Abubakar al-Baghdadi, baadhi ya wataalam wanasema alikuwa mjumbe wa chama cha Baas cha kiongozi wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein. Alijiunga na al Qaeda baada ya uvamizi wa Marekani. Hadji Moutazz alikamatwa mwaka 2005, na alikabidhiwa viongozi wa Iraq ambao baadae walimuachilia huru. Kifo chake kilikua kilitangaza na Pentagon mwezi Desemba mwaka 2014, lakini taarifa hiyo ilionekana kuwa ni uongo.

Kwa mujibu wa Ned Bei, msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani, kifo chake kiongozi huyo wa Islamic State kitasababisha athari kubwa katika shughuli za kundi la Islamic State. Lakini Christopher Hamer, mchambuzi wa masuala ya kijeshi amesema bado ana mashaka. Katika kurasa za gazeti la Los Angeles Times, inasadikiwa kuwa kundi la Islamic State liliajiri maafisa wengi wa zamani wa Saddam Hussein, wenye uwezo ambao wanaweza kuchukua nafasi yake, amearifu mwandishi wetu mjini Washington, Jean-Louis Pourtet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.