Pata taarifa kuu
Iraq - mashambulizi

Irak yatathumini taarifa za kujeruhiwa kwa Al Baghdad

Idara ya ujasusi nchini Irak inaendesha uchunguzi kuhusu uwepo wa taarifa za kushambuliwa na kujeruhiwa kwa kiongozi mkuu wa kundi linalo jiita Islamic State Abou Bakar al Baghdadi katika mashambulizi ya anga.

gari la kijeshi la Iraq katika mji wa Ramadi
gari la kijeshi la Iraq katika mji wa Ramadi REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Saad Maan amesema wanakusanya taarifa kutoka huku na kule ili kufanya tathmini kuhusu taarifa hii

Hapo jana Jumapili jeshi la Israel lilifahamisha katika taarifa yake kwamba msafara wa kiongozi wa kundi linalo jiita Islamic State ulishambuliwa wakati ukielekea katika jimbo la Karabla karibu na mpaka na Syria ambako kulitarajiwa kufanyika mkutano wa viongozi wenye msimamo mkali wa kundi hilo.

Kulingana na taarifa hiyo, jengo ambalo lingepokea mkutano huo nalo pia limeshambuliwa na vikosi vya jeshi la Irak na ambapo hali ya afya ya kiongozi wa kundi hilo haijulikani ilivyo kwa sasa.

Jeshi la Irak liliwahi kutangaza kuwa kiongozi wa kundi hilo amejeruhiwa na huenda ameuawa, lakini hadi leo haijawahi kuthibitishwa mbali na kluonekana kwamba sio kweli.

Viongozi wa kidini wa jimbo la kisunni la Al Anbar magharibi wanasema kwa upande wao kwamba wanazo taarifa kuwa kiongozi wa kundi la Islamci State alijeruhiwa katika masahmbulizi ya anga, huku ma chifu kadhaa wa Daesh wakipoteza maisha.

Taarifa kutoka kwa wananchi wa mji wa Karabla zaleza kwamba Al Baghdadi na viongozi wengine walisafirishwa katika Hospital iliopo katika mji wa Albu Kamal mji uliopo karibu na mpaka wa Irak na Israel.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.