Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Waisrael 4 wajeruhiwa katika shambulizi la kisu kusini mwa Israel

Waisrael 4 wamejeruhiwa katika shambulio la kisu lililotekelezwa leo Jumamosi katika mji wa Kiryat Gat kusini mwa Israeli, polisi ya Israel imetangaza.

Askari wa Israel wakipiga doria karibu na mji wa Beit Hadassah katika eneo la Hebroni Oktoba 29, 2015.
Askari wa Israel wakipiga doria karibu na mji wa Beit Hadassah katika eneo la Hebroni Oktoba 29, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Waisrael hao 4 ni Wayahudi, na mmoja wao alijeruhiwa vibaya, vyanzo vya matibabu vimebaini.Miongoni mwa watatu, mmoja anasumbuliwa na majeraha madogo tu.

Polisi imelitaja shambulizi hilo kuwa ni la "kigaidi", na kuongeza kuwa imeanza kumsaka msambuliaji ambaye alitimka baada ya kitendo hicho, na kwa sasa hajulikani aliko.

Mashambulizi ya visu yamekithiri katika Ukanda huo hususan katika Ukingo wa Magharibi, na katika mji wa Jerusalem (Mashariki).

Mashambulizi haya ya visu, makabilano kati ya vijana wa Palestina na askari wa Israel na vurugu kati ya wakazi wa Palestina na walowezi wa Israel yamewaua Wapalestina 86, ikiwa ni pamoja na Muisrael mwenye asili ya Kiarabu na Waisrael 15 pamoja na Mmarekani mmoja na raia mmoja wa Eritrea , kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.