Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Bobi Wine asita kuwasilisha madai ya udanganyifu mbele ya Mahakama

Baada ya wanajeshi kuondoka nyumbani kwa mkosoaji mkubwa wa rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa amri ya mahakama, Bobi Wine amendelea kupinga matokeo ya uchaguzi, lakini hata hivyo akisita kuweka wazi kama atawasilisha malalamiko yake mbe ya Mahakama Kuu.

Robert Kyangulanyi, maarufu kama  Bobi Wine, akiwa katikati ya wafausi wake katika siku zilizopita
Robert Kyangulanyi, maarufu kama Bobi Wine, akiwa katikati ya wafausi wake katika siku zilizopita SUMY SADURNI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bobi Wine amezungumza na waandishi wa habari na maafisa wa chama chake nyumbani kwake Magere baada ya wanajeshi kuondoka nyumbani kwake.

Ingawa kwa mara nyingine amekashifu udanganyifu wa uchaguzi na kukataa matokeo ya uchaguzi huo, bado anasita kupinga uchaguzi mahakamani.

Bado hakuna jibu la wazi juu ya uamuzi wa Bobi Wine ikiwa atakata rufaa au la kupinga matokeo ya uchaguzi mbele ya Mahakama Kuu. Kulingana na mpinzani huyo, mjadala bado unaendelea ndani ya chama chake:

"Kwanza, nataka kuwambia kuwa tuna ushahidi wakutosha, kulingana na kutofautiana kwa takwimu. Tuliwaambia kuwa tunafanya mazungumzo na wenzetu juu ya jinsi ya kuendelea na utaratibu wa kuwasilisha madai yetu mbele ya Mahakama hiyo iliyoundwa na Jenerali Museveni. Lakini ikiwa tutaenda mahakamani, itakuwa vita vipya kuweka hatarini utawala huo. "

Bobi Wine ameeelezea kwamba anahofia kwamba mahakama inaweza kuwa na upendeleo katika uamuzi wake. Chaguzi tatu zilipingwa mahakamani bila mafanikio yoyote tangu Rais Yoweri Museveni aingie madarakani.

Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 38 alikuwa katika kizuizi cha nyumbani tangu siku ya uchaguzi mkuu wa Januari 14, baada ya vikosi vya usalama kudai kuwa vilikwenda kwenye makaazi yake kwa ajili ya kumlinda.

Uchaguzi huo mkuu wa Uganda, ulimpa ushindi Rais Yoweri Museveni, matokeo ambayo yamepingwa na Bobi Wine, akidai kuwa uligubikwa na udanganyifu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.