Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Bobi Wine asema Ofisi ya chama chake kimevamiwa na jeshi

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na aliyekuwa mgombea urais Bobi Wine amesema wanajeshi wamevamia Ofisi za chama chake cha NUP, wakati maafisa wa chama hicho walipokuwa wanaendelea na kazi ya kukusanya ushahidi kwenda Mahakamani kupinga ushindi wa rais Yoweri Museveni baada ya Uchaguzi Mkuu wiki iliyopita.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine AFP Photos/ Guillem Sartorio
Matangazo ya kibiashara

Wakati uo huo, Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imetaka uchunguzi wa kina na wa wazi, kufanyika kuhusu madai ya wizi wa kura nchini humo.

Bobi Wine ameedelea kusema kuwa yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi huo na kulaani kuendelea kuzuiwa nyumbani kwake.

Rais Museveni, alitangazwa kuwa mshindi Jumamosi iliyopita, kwa kupata ushindi wa asilimia asilimia 58.6 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Bobi Wine aliyepata asilia 34.8.

Wanajeshi wamezingira makaazi yake kutoka siku ya Ijumaa kwa kile wanachosema ni kumpa ulinzi.

Uchaguzi nchini Uganda umefanyika kwa mazingira magumu, kufuatia kufungwa kwa mitandao ya kijamii na Internet lakini mtandao huo ulifunguliwa siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.