Pata taarifa kuu
UGANDA-BOBI WINE-UCHAGUZI UGANDA 2021

Polisi Uganda yajuta kufuatia mauaji ya wafuasi 50 wa upinzani

Polisi nchini Uganda sasa wanasema wanajuta kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji wa mgombea urais kupitia chama cha upinzani cha Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

Mgombea urais nchini Uganda, Bobi Wine.
Mgombea urais nchini Uganda, Bobi Wine. AFP Photos/ Guillem Sartorio
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa polisi anayesimamia operesheni nchini humo Edward Ochom ameomba msamaha baada ya kikao na viongozi wa dini waliomtembelea katika makao ya jeshi hilo la Polisi.

Katika hatua nyingine, Tume ya uchaguzi imembadilishia walinzi Bobi wine, siku moja tu baada ya kiongozi wa walinzi wa Kyagulanyi na msaidizi wake,kupingwa risasi za mipira.

Miaka 12 iliyopita, Bobi Wine alikuwa akijulikana kwa kuimba nyimbo zinazoeleza maisha ya watu masikini - yeye mwenyewe akiwa amezaliwa na kukulia katika mazingira ya kimasikini huko Kamwokya, na hilo ndilo jambo lililompa umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi wa taifa hilo ambao wengi wao ni masikini.

Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Uchaguzi ya Uganda, asilimia 80 ya wapiga kura wa taifa hilo katika uchaguzi huo wana umri wa kati ya miaka 18 hadi 40; umri ambao Bobi Wine anaangukia.

Ni asilimia 1.7 tu ya wapiga kura wa Uganda wana umri wa zaidi ya miaka 70.

Takwimu hizo zinaonyesha pia kwamba watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea - ambao angalau wameona mafanikio ya utawala wa Museveni katika maisha yao, wanafikia asilimia 13 ya wapiga kura wote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.