Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA-WAKIMBIZI-USALAMA

Wasiwasi watanda katika kambi za wakimbizi Warundi Tanzania

Zoezi la kuwarejesha Burundi wakimbizi wa nchi hiyo walioko kwenye kambi za wakimbizi nchini Tanzania linaendelea, licha ya ukinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wakimbizi wasiotaka kurejeshwa.

Kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania (Picha ya kumbukumbu)
Kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania (Picha ya kumbukumbu) Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali za Burundi na Tanzania mwezi Agosti, zilikubaliana kuwa wakimbizi zaidi ya 200,000 ambao wamekuwa wakiishi nchini Tanzania wataanza kurudi nyumbani kuanzia tarehe 1 mwezi Oktoba.

Nestor Bimenyimana, Afisa wa juu wa serkali ya Burundi anayehusika na mradi wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi, ameliambia Shirika la Habari la Uingereza la Reuters kuwa mpango huo utaanza kutekelezwa baada ya makubaliano ya serikali yake na Tanzania.

Aidha, amesema kuwa kundi la kwanza, litawajumuisha wakimbizi 1,000 ambao Bimenyimana, amesema wanaorudi, na ambao wanafanya hivyo kwa hiari yao.

Hata hivyo duru kutoka kwa baadhi ya wakimbizi zinasema kuwa wakimbizi zaidi ya 900 wametakiwa kujiorodhesha mbele ya mamlaka husika nchini Tanzania.

Wakimbizi wanasema wana wasiwasi kuwa zoezi la kuwarudisha makwao sasa limeanza, na “wana hofu ya kurudishwa Burundi kwa nguvu.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikilaumiwa kutaka kuwarejesha makwao wakimbizi kwa nguvu. Wanaharakati wa Haki za Binadamu wanaishtumu Tanzania kufanya mpango wa siri na serikali ya Burundi kwa kuwarejesha kwa nguvu wakimbizi Warundi waishio nchini Tanzania.

Mnamo mwezi Agosti Serikali ya Tanzania iliagiza wakimbizi kutoka nchini Burundi kurudishwa makwao, na kusema kua hali ya kiusalama katika taifa hilo sasa imeimarika.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola alitangaza kuwa wakimbizi 2,000 watarudishwa Burundi kufikia Oktoba mosi.

Tanzania imekuwa inalinyooshea kidole cha lawama shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR kwamba ndio linakataa wakimbizi hao kurudishwa nchini Burundi.

Tanzania inashikilia kuwa sababu iliyoifanya kuwapatia hadhi ya ukimbizi raia hao wa Burundi kwa sasa hazipo na kwamba ina kila sababu ya kuwataka warudi makwao.

Mvutano kati ya shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa mataifa na serikali ya Tanzania kuhusu suala la kuwarejesha makwao wakimbizi wa Burundi umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa.

Mwezi Agosti mwaka mwaka 2017, Serikali ya Tanzania ililipatia shirika la UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali ifanye zoezi hilo yenyewe.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.