Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-MAASKOFU-KATOLIKI-UCHAGUZI 2020

Kanisa Katoliki nchini Burundi laishtumu serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Burundi linasema linahofia ongezeko la visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu na wapinzani kusumbuliwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao, wakati huu serikali nchini humo ikiwashtumu maaskofu hao kwa kuhubiri chuki.

Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Jumapili iliyopita, ujumbe wa maaskofu ulisomwa Makanisani kulalamikia ongezeko la visa hivyo vinavyowalenga wapinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

“Kumeendelea kushuhudiwa kwa visa vinavyowalenga wanasiasa wa upinzani, wenye maoni tofauti na serikali,”ujumbe huo ulieleza.

Shutuma hizi zimekuja, baada ya mapema mwezi huu ripoti ya watalaam wa Umoja wa Mataifa kumshtumu rais Pierre Nkurunziza kwa kuhusika binafsi katika ukiukwaji wa visa hivyo.

Mwaka 2015, mzozo wa kisiasa ulisababisha zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine zaidi ya 400,000 kuyakimbia makwao baada ya rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu kinyume cha Katiba.

Mwaka 2018, kulikuwa na mabadiliko ya Katiba ambayo yatamwezesha rais Nkurunziza kuendelea kuwa madarakani hadi mwaka 2034.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.