Pata taarifa kuu
UGANDA-SUDANI-KUSINI

Uganda kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Sudan Kusini

Uganda imesema itaanza kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoishi nchini humo kuanzia mwezi Januari mwaka 2019. Kauli hii imetolewa na rais wa Yoweri Museveni, wakati akiwa katika ziara ya siku moja nchini Tanzania, alipokutana na rais wa nchi hiyo John Magufuli jijini Dar es Salaam.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi azuru kambi ya wakimbizi ya Adjumani kaskazini mwa Uganda Agosti 20, 2016.
Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi azuru kambi ya wakimbizi ya Adjumani kaskazini mwa Uganda Agosti 20, 2016. Charlotte Cosset / RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wiki iliyopita, kutia saini mkataba wa kugawana madaraka jijini Khartoum nchini Sudan.

Wakati huo huo, Tanzania imethibitisha kuwa wakimbizi kutoka Burundi ambao wanaishi nchini humo wameanza kurejea nyumbani kwa hiari.

Rais Magufuli amesema, hii inatokana na hali ya amani kuanza kurejea katika nchi yao.

Mbali na masuala hayo ya kikanda, viongozi hao wawili wamejadiliana kuhusu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania, na kuwataka maafisa wa nchi hizo mbili kuharakisha mradi huo.

Pamoja na hilo, Uganda na Tanzania zimekubaliana kujenga reli ya kati itakayounganisha nchi hizo mbili kutokea Mwanza lakini pia kupambana biashara ya sukari ya magendo inayotishia kuharibu soka la mataufa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.