Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-MACHAR-KIIR-MSAMAHA

Rais Kiir atoa msamaha kwa Machar na makundi ya waasi

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametangaza msamaha kwa makundi yote ya waasi akiwemo hasimu wake Riek Machar ambaye ni kiongozi wa waasi hao.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Kiir ametoa tangazo hili kupitia redio ya taifa, siku chache baada ya kutia saini mkataba wa amani wa namna ya kugawana madaraka na Machar jijini Khartoum nchini Sudan.

Msamaha huu unaanza tayari umeanza kutekelezwa.

“Rais Salva Kiir ametoa msamaha dhidi ya Dokta Riek Machar na makundi mengine ya waasi ambayo yamekuwa yakipambana na serikali tangu mwaka 2013. Msamaha huu unaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 8 mwezi Agosti 2018,” Tangazo lililosomwa kupitia Redio ya Taifa.

Aidha, Kiir amewataka wanajeshi wanaomuunga mkono kutekeleza mkataba wa kusitisha makabiliano yoyote dhidi ya vikosi vya Machar.

Mkataba wa mwisho unatarajiwa kutiwa saini hivi karibuni,ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya mpito itakayoundwa baada ya miezi mitatu na kuongoza kwa miezi 36 kabla ya Uchaguzi Mkuu kufanyika.

Riek Machar, anatarajiwa kurejea katika wadhifa wa Makamu wa kwanza wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.