Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI-UCHUMI

Museveni ajitetea kuhusu sheria tata inayowatoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametetea sheria mpya, inayowezesha watumiaji wa mitandao ya kijamii kutozwa kodi kila siku. Museveni amesema Waganda wamekuwa wakitumia mitando hiyo kusema uongo, kupoteza muda na kujiburudisha.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni Capture d'écran al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Watumiaji wa mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na nyingine, wanalazimika kulipia Shilingi 200 za Uganda kila siku, fedha ambazo rais Museveni amesema zitasaidia katika maendeleo ya nchi.

Wanaharakati wamekwenda Mahakamani kupinga sheria.

Wananchi wa Uganda wameendelea kuilalamikia serikali ya nchi yao kuhusu hatua hiyo mpya iliopitishwa hivi majuzi na bunge kupitisha muswada tata wa kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii na huduma za miamala ya kifedha kwa njia ya simu.

Hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF) lililaani kikwazo cha kukusanya taarifa na kuripoti nchini Uganda kufuatia sheria mpya inayotoza kodi ya kila siku kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa walioguswa na sheria hiyo ni wamiliki wa blogu na waandishi wa habari ambao bado wanatumia mitandao ya kijamii kujieleza kwa uhuru zaidi kuliko katika vyombo vingine vya habari nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.