Wanaharakati wapinga hatua ya serikali kuhusu kodi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
Wanaharakati nchini Uganda wamekwenda katika Mahakama ya Kikatiba, kupinga utekelezwaji wa sheria inayowatuza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo.
Imechapishwa:
Sheria hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 1 mwezi huu ambayo watumiaji wa mitandao hiyo, walianza kulipia Shilingi 200 kwa siku.
Wanaharakati hao wakiongozwa na Mawakili wanne ambao ni vijana, wanaitaka Mahakama kuamua kuwa sheria hiyo ni kinyume cha Katiba na inakiuka haki za binadamu.
Hii imekuja baada ya bunge mwezi uliipita kupitisha sheria na kuwepo kwa utozwaji ushuru kwa wale wanaotumia mitandao hiyo kama Facebook, Twitter,Instagram, Youtube na Skype miongoni mwa mingine.
Serikali ya rais Yoweri Museveni imesema, fedha zitakazopatikana zitasaidia kufadhili maendeleo mbalimbali.