Pata taarifa kuu
KENYA-VYOMBO VYA HABARI

Kenyatta atia saini muswada tata kuhusu makosa ya mtandao

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini muswada tata wa makosa ya mtandao kuwa sheria licha ya pingamizi kubwa kutoka kwa wanahabari na watetezi wa haki za binadamu.

Rais Uhuru Kenyatta akitia saini muswada kuhusuwa makosa ya mtandao.
Rais Uhuru Kenyatta akitia saini muswada kuhusuwa makosa ya mtandao. RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Sheria hii mpya inawalenga wanahabari na wale wanaotumia mitandao ya kijamii watakaopatikana na kosa la kuchapisha habari za uongo lakini pia kwa watumizi wa mitandao mbalibali ya kijamii wanaosambaza picha za uchi.

Atakayevunja sheria hii mpya, atakamatwa na kufikishwa Mahakamani na kulipa faini ya Shilingi za nchi hiyo Milioni tano au kufungwa jela miaka miwili.

Lakini wale walio na tabia ya kuandika matusi au maneno ya kumdhalilisha mwingine pia watajipata matatani kwa mujibu wa sheria.

Mbali na hilo, yeyote atakayechapisha habari za uongo na kusababisha hofu au machafuko nchini humo, atafungwa jela miaka 10.

Hatua ya rais Kenyatta imekuja baada ya Kamati ya Kimataifa ya kutetea wanahabari CPJ, kutoa wito kwa kiongozi wa nchi hiyo kutotia saini sheria hiyo kwa sababu inalenga kuminya uhuru wa wanahabari.

Hata hivyo, wabunge wamejitetea na kusema kuwa sheria hiyo itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao na uhalifu unaoweza kutokea na kusababisha uvunjifu wa amani katika taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.