Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-SIASA

Tume ya Uchaguzi Kenya yakumbwa na kizungumkuti

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC kwa sasa haiwezi kuendelea na shughuli zozote baada ya kujiuzulu kwa Makamishna watatu siku ya Jumatatu wiki hii.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati, akitamngaza mshindi wa uchaguzi wa urais, Nairobi, Oktoba 30, 2017.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC), Wafula Chebukati, akitamngaza mshindi wa uchaguzi wa urais, Nairobi, Oktoba 30, 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Makamishna hao wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti Connie Maina , Paul Kurgat na Margaret Mwachanya, walisema walichukua hatua hiyo kwa kile walichosema Mwenyekiti Wafula Chebukati ameshindwa kuongoza Tume hiyo.

Sheria za Uchaguzi nchini Kenya, zinaeleza kuwa Makamishna watano kati ya saba ndani ya Tume hiyo ndio wanaoweza kufanya maamuzi yoyote lakini kwa sasa hili litakuwa vigumu kwa sababu, waliosalia ni watatu.

Mwenyekiti Wafula Chebukati amesema hajapokea rasmi barua ya kujiuzulu kwa Makamishena hao wa zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.