Pata taarifa kuu
KENYA-MGOMO-ELIMU

Vyuo vikuu vya umma kukabiliwa na mgomo Kenya

Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya umma nchini Kenya, wameanza mgomo kwa kile wanachosema, serikali imeshindwa kutekeleza mkataba wa kuwaongezea mshahara kama ilivyokubaliwa mwaka uliopita.

Chuo Kikuu cha Sheria cha Nairobi Kenya.
Chuo Kikuu cha Sheria cha Nairobi Kenya. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Constatine Wasonga, Katibu Mkuu wa muungano wa wahadhiri nchini humo UASU, amesema serikali imeshindwa kuheshimu makubaliano waliofikia na imewadharau.

Mgomo huu utasababisha zaidi ya wananfunzi Laki 6 kukaa nyumbani.

Katika miaka ya hivi karibuni Kenya ilikabiliwa na migomo ya hapa na pale, hasa katika sekta ya afya na elimu.

Migomo hiyo mara nyingi imekua ikisababishwa na suala la nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi katika sekta hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.