Serikali nchini Kenya yasema bweni la wanafunzi liliteketezwa makusudi
Waziri wa Elimu nchini Kenya Fred Matiang'i amesema moto uliozuka katika bweni la Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Moi jijini Nairobi, na kusababisha vifo vya wanafunzi tisa na wengine kujeruhiwa ulianzishwa kwa makusudi.
Imechapishwa:
Matiang'i ameeleza kuwa uchunguzi wa awali umeonesha wazi kuwa, mkasa huo haukuwa ajali na tayari polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Aidha, Waziri huyo ambaye pia anakaimu kama Waziri wa Usalama, ameeleza kuwa Polisi wamemfahamisha kuwa wamepata taarifa za uhakika kuonesha kuwa moto huo ulianzishwa makusudi.
Shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili, wakati huu wanafunzi, wazazi na walimu wakiendelea kuomboleza.
Mwaka uliopata, mabweni ya shule za sekondari 100 yaliteketezwa moto katika visa ambavyo pia viliripotiwa kuwa vya makusudi.