Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Upinzani kufikisha malalamiko yake mahakamani Uganda

Wabunge wa upinzani nchini Uganda wanajiandaa kuwasilisha maombi yao kwenye Mahakama ya Katiba kuiomba kutoidhinisha sheria ambayo rais Museveni aliidhinisha hivi karibuni.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika moja ya makazi yake Rwakitura, magharibi mwa Uganda mnamo Februari 21, 2016.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika moja ya makazi yake Rwakitura, magharibi mwa Uganda mnamo Februari 21, 2016. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mageuzi haya ya kikatiba yaliondoa kikomo cha umri wa rais.

Hii inamaanisha kuwa rais Yoweri Kaguta Museveni, madarakani tangu mwaka 1986, atawania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021. Wakati huo atakua ametimiza rasmi umri wa miaka 77. Upinzani haupingi tu matokeo, lakini utaratibu, wabunge waliopigwa au kulipwa, askari waliojihami kwa silaha kuletwa ndani ya jengo la bunge. Hayo yanajiri wakati ambapo jumuiya ya kimataifa ikiendelea kusalia kimya.

Upinzani nchini Uganda na mashirika ya kiraia yamekosoa mwenendo huo wa jumuiya ya kimataifa.

Hali hii imeendelea kushuhudiwa nchini Uganda. Mwaka 2005 rais yoweri Museveni alijaribu kufanya mageuzi ya katiba bila wasiwasi wowote wala kuchukuliwa vikwazo vyovyote, wakati ambapo hangeliweza kuwania kwa muhula wa pili, kulingana na katiba ya wakati huo. Bw Museveni hajachukuliwa vikwazo ndani na nje ya nchi na hivyo kuvunja sheria, jumuiya ya kimataifa ikishuhudia.

"Rais Museveni ni kama rais wa Rwanda Paul Kagame, anaua bila wasiwasi, anavunja sheria, anaiba mali za DRC, akiungwa mkono na Marekani, huku nchi kama hizo zikiendelea kupata misaada," ameonya mwangalizi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Hii ni hoja ambayo mtafiti na mwandishi wa habari Helen Epstein ameiendelea katika kitabu chake kijulikanacho kama Marekani, Uganda na vita dhidi ya ugaidi. Kuanzia miaka ya kwanza, baada ya mapinduzi, Yoweri Museveni alijiweka karibu na Marekani, mwanafunzi mzuri wa vita dhidi ya ugaidi hata kabla ya tukio baya lililotokea Septemba 11 nchini Maekani. Tangu wakati huo, amepokea jumla ya bilioni 20 za misaada ya maendeleo, bilioni 4, ya kufuta madeni, msaada wa kijeshi, wa kifedha, vifaa, mafunzo, labda muhimu sana, haijulikani kiwango.

Na msaada huo si kutoka tu Marekani, hata Uingereza, au Ufaransa, wanaisadia Uganda. Na kutokana na misaada hiyo jeshi la Uganda linachukuliwa kwa sasa kama jeshi lenye nguvu zaidi barani Afrika, licha ya vitendo viovu linaloshtumiwa. Jeshi hili pia linafaulu pakubwa kutokan ana kutumwa kwake nchini Somalia dhidi ya wapiganaji wa Al Shabab. "Museveni, kama Kagame, ni moja ya nguzo muhimu ya utulivu, hata kama ni maono ya muda mfupi," chanzo cha kidiplomasia kimepongeza.

Kwa upande wa kiongozi wa Upinzani katika bunge la Uganda, anasema hali hiyo haishangazi

Ibrahim Ssemujju anasema hatarajii chochote: "wakati Museveni anatuma askari nchini Somalia kupambana katika vita vyao, jumuiya ya kimataifa inafumbia macho kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu au sheria nchini Uganda. Kwa hivyo hatuwezi kutarajia msaada wowote kutoka kwa nchi hizi, hatuna matumaini yoyote ya msaada kutoka kwao."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.