Pata taarifa kuu
UGANDA

Uganda: Bunge lakosolewa kuondoa kipengele cha umri wa rais kwenye katiba

Wabunge nchini Uganda wamepitisha muswada wa mabadiliko ya katiba kuondoa kipengele cha ukomo wa umri kwa mtu atakayewania urais, hatua inayotoa nafasi sasa kwa rais Yoweri Kaguta Museveni kuhudumu kwa muhula wa sita madarakani.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni GAEL GRILHOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Muswada huu tata uliopitishwa uliungwa mkono na wabunge 315, wakati wabunge 62 wakiupinga wengi wakitoka upinzani na wachache kutoka chama tawala.

Hatua hii ilifikiwa baada ya siku tatu za wabunge kujadiliana huku kukishuhudiwa ulinzi mkali ndani na nje ya bunge ambapo wakati fulani hata wabunge wenyewe walivutana mashati.

Muswada huu sasa utakuwa sheria baada ya rais Yoweri Museveni kuutia saini.

Chini ya sheria ya sasa rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 asingeweza kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2021 kwa kuwa katiba iliweka ukomo wa mtu kuwa rais akifikisha miaka 75.

Muswada huu mpya pia umerejesha ukomo wa mihula ya rais kuwa madarakani, sheria ambayo iliondolewa wakati katika ilipofanyiwa marekebisho wakati wa kuingizwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 2005.

Hii inamaanisha kuwa katika uchaguzi ujao rais Museveni ataweza kuwania urais kwa mihula mwili ambapo akichaguliwa atakaa madarakani mpaka mwaka 2031.

Katika mabadiliko mengine yaliyopitishwa ni pamoja na kuongezwa kwa muda wa wabunge kuhudumu kutoka miaka mitano hadi saba, ambapo sasa uchaguzi wa wabunge utafanyika mwaka 2023.

Wanaharakati wa haki za binadamu wamekosoa hatua ya bunge ambayo wamesema inarudisha nyuma demokrasia ya nchi hiyo na maamuzi ya wananchi.

Msemaji wa chama tawala cha NRM Rogers Mulindwa amekanusha madai kuwa kubadilishwa kwa kipengele cha umri kwenye katiba kulilenga kumnufaisha rais Museveni.

Spokesman for the ruling National Resistance Movement (NRM) party Rogers Mulindwa denied that the law was designed to benefit Museveni personally.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.