Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UN-USALAMA-USHIRIKIANO

UNMISS: Hakuna juhudi zozote kutoka upande wa serikali

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa linasema serikali ya Sudan Kusini haijaonesha juhudi zozote za kuunga mkono pendekezo la Marekani la kuwa na jeshi la ukanda la kulinda amani.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano IGAD, Machi 25, 2017, Nairobi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano IGAD, Machi 25, 2017, Nairobi. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hili limewahi kutolewa na nchi za Afrika Mashariki IGAD ambazo zimekuwa zikitaka kutumwa kwa wanajeshi hao wa kulinda amani kwa lengo la kuwalinda raia.

Umoja wa Mataifa unasema, licha ya rais Salva Kiir kuahidi kuunga mkono juhudi hizo, hilo halijatekelezwa.

Hayo yanajiri wakati ambapo kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, wiki hii, alisema mazungumzo ya kitaifa yanayoendelea nchini mwake hayana maana yoyote na badala yake anataka mazungumzo hayo yaongozwe na muungano wa nchi za IGAD.

Machar alimwambia Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuwa, haamini kuwa mazungumzo yanayofanyika nchini Sudan Kusini yanaweza kuzaa matunda yoyote.

Rais Salva Kiir kwa upande wake amekuwa akisema kuwa, mazungumzo pekee yatakayoleta mwafaka ni yale ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.