Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Sudan Kusini haiko tayari kuandaa Uchaguzi Mkuu

Shirika la kiraia linaloshughulikia masuala ya Demokrasia na Uchaguzi nchini Sudan Kusini linasema nchi hiyo haiko tayari kuandaa  Uchaguzi Mkuu.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Jok Solomon
Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo linalojiita kama SsuNDE, limesema kuwa Uchaguzi huo hauwezi kufanyika mwaka ujao kwa sababu vita bado vinaendelea katika maeneo mengi nchini humo.

Kauli hii imekuja baada ya Waziri wa Habari Michael Makuei ambaye amenukuliwa akisema kuwa, taifa hilo lipo tayari kuandaa Uchaguzi mwaka ujao.

Makuei ameongeza  kuwa, nchi hiyo itaendelea na zoezi hilo pamoja na kwamba  bado inakabiliwa na changamoto za kiusalama.

Kwa mujibu wa mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2015, jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, Uchaguzi mpya ulitarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Mkataba huo haujatekelezwa ipasavyo kwa sababu, kiongozi wa upinzani Riek Machar amekimbilia  nchini Afrika Kusini.

Mamilioni ya raia wa nchi hiyo wamekimbia makwao huku maelfu wakipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.