Pata taarifa kuu
UGANDA-SAISA

Bunge kukutana tena Jumatano hii nchini Uganda

Wabunge nchini Uganda wanatarajiwa kurejea bungeni leo saa nane mchana kujadili na kupitisha au la mswada wa kuibadlisha Katiba.

Kikao cha bunge kiliahirishwa baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga shughuli za bunge na kuzuia wabunge wa chama tawala cha NRM kushindwa kuwasilisha mswada wa kuibadlisha Katiba.
Kikao cha bunge kiliahirishwa baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga shughuli za bunge na kuzuia wabunge wa chama tawala cha NRM kushindwa kuwasilisha mswada wa kuibadlisha Katiba. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Kikao cha jana kiliahirishwa baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga shughuli za bunge hilo na kuzuia wabunge wa chama tawala cha NRM kushindwa kuwasilisha mswada wa kuibadlisha Katiba.

Wabunge wa NRM wanataka Katiba kubadalishwa ili kifungu kinachomzuia mtu kuwania urais akiwa na zaidi ya miaka 75 kuondolewa.

Hata hivyo, wabunge wa upinzani ambao jana walivuruga shughuli za bunge kwa kuimba wimbo wa taifa wakiwa wamejifunga vitambaa vyekundu, wameapa kutoruhusu mabadiliko hayo.

Wabunge wa upinzani nchini Uganda kwa mara nyingine tena jana walifanikiwa kuzuia wabunge wa chama tawala wasilisha ombi la kutaka kuandaliwa kwa mswada wa kubadilisha Katiba ya nchi hiyo ili kuondoa kifungu kinachozuia mtu yoyote kuwania urais akiwa zaidi ya miaka 75.

Mwaka 2012 wakati akihojiwa na kituo cha NTV Uganda, rais Museveni alinukuliwa akisema haamini kuwa kiongozi anaweza kuwa na uwezo wa kufanya kazi vema akiwa na zaidi ya miaka 75.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.