Pata taarifa kuu
UGANDA-WABUNGE

Wabunge wa chama tawala nchini Uganda kujaribu tena kuomba kubadilisha Katiba

Mvutano mwingine unatarajiwa kushuhudiwa tena katika bunge la Uganda wakati wabunge wa chama tawala NRM, watakapojaribu kuwasilisha ombi la kuandaa mswada wa kubadilisha Katiba ya nchi hiyo.

Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda Muhammad Nsereko na  Allan Sewanyana
Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda Muhammad Nsereko na Allan Sewanyana Charlotte Cosset/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa NRM wanataka kubadilishwa kwa kifungu cha katiba cha 102, ibara ya b, ili kuondoa kikomo cha umri wa mgombea urais nchini humo.

Hatua hii inakuja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021, ikitarajiwa kuwa iwapo mabadiliko hayo yatafanyika, rais Yoweri Museveni atakayekuwa na umri wa miaka 76, atawania tena urais .

Katiba ya Uganda inaeleza kuwa, mtu hawezi kuwania urais akiwa na umri wa miaka 75 na zaidi, kifungu ambacho wabunge wa NRM wanataka kiondolewe.

Mchambuzi wa siasa Kenneth Lukwago akiwa jijini Kampala, amekuwa akiiambia RFI Kiswahili kuwa chama cha NRM kinaona kuwa hakuna mtu anayeweza kuwania urais mwaka 2021 kupitia chama hicho.

Pamoja na hilo, chama cha NRM kinaona kuwa njia pekee ya kuendelea kuwa madarakani ni kwa rais Museveni kuwania tena urais.

Aidha, kuna wale wanaona kuwa rais Museveni ameongeza vema kwa zaidi ya miaka 30 na kutoa mfano wa kuimarika kwa hali ya usalama na amani hasa Kaskazini nchini humo na hivyo anastahili kuendelea kuongoza.

Hata hivyo, wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Kizza Besigye wameapa kutoruhusu mabadiliko hayo huku wakisema hawataki katiba kubadilishwa.

Siku ya Jumnne, hali ya usalama uliimarishwa nje ya bunge la jiji la Kampala na hasa maeneo ya bunge kuelekea vikao vya bunge.

Maandamano ya kupinga mabadiliko hayo pia yanatarajiwa kushuhudiwa.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.