Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-AL SHABAB

Al Shabab yawauwa watu 9 katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya

Kundi la kigaidi la Al Shabab kutoka Somalia, limewauwa watu tisa katika Kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya.

Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za maafisa wa Polisi zinasema kuwa,mauaji hayo yalifanyika katika vijiji vya Jima na Pandaguo karibu na mpaka wa Somalia kwa wanamgambo hao kuwapiga risasi na kuwakata shingo.

Watu wote waliopoteza maisha katika shambulizi hili ni raia wa kawaida kwa mujibu wa ripoti za Polisi.

Mapema wiki hii, kundi la Al Shabab lilishambulia kituo cha Polisi katika eneo la Pandaguo na kusababisha vifo vya maafisa watatu.

Shambuli hili limekuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kuomboleza kifo cha Waziri wa Usalama, Joseph Nkaiserry.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa nafasi hiyo itashikiliwa kwa muda na Waziri wa Elimu Fred Matiang'i.

Al Shabab ilianza kushambulia Kenya tangu mwaka 2011, baada ya kutuma jeshi lake nchini humo kwenda kupambana na wanamgambo hao na baadaye kuungana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika AMISOM.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.