Pata taarifa kuu
TANZANIA

Baadhi ya maeneo nchini Tanzania yakabiliwa na baa la njaa

Baadhi ya maeneo nchini Tanzania yanakabiliwa na baa la njaa, kutokana na kile ambacho wataalam wanasema ni kwa sababu ya ukame unaoshuhudiwa.

Mkulima akivuna mazao yake nchini Tanzania
Mkulima akivuna mazao yake nchini Tanzania www.wfp.org
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya maeneo nchini Tanzania yamekuwa yakishuhudia kiasi kidogo cha mvua, kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Maeneo yanayotajwa kukabiliwa na hali hii ni pamoja na Simiyu, Bunda, Musoma, Kagera na maeneo mengine ya Pwani kama Chalinze na Morogoro na kusababisha mifugo kufa kwa njaa kutokana na ukosefu wa malisho.

Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa, bei ya vyakula kama mahindi, unga, ndizi na miongoni mwa vyakula vingine ambavyo bei yake imepanda maradufu.

Hivi karibuni, Waziri wa fedha nchini humo Philip Mpango, alitaja sekta ya kilimo nchini humo inayochangia ukuaji wa pato la taifa kukua polepole sana katika miaka ya hivi karibuni ambayo ni kati ya asilimia 2.7 hadi 0.3.

Rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli, akiwa ziarani mkoani Kagera eneo ambalo linakabiliwa na baa la njaa, aliwaambia viongozi wa eneo hilo wahakikishe kuwa wananchi wana chakula cha kutosha.

Hata hivyo, Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP), linasema kuwa Tanzania ambayo ina zaidi ya watu Milioni 50 na inaendelea kuwa na chakula cha kutosha kitaifa licha ya baadhi ya maeneo kukabiliwa na baa la njaa.

Asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.